Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa anasaka mtu atakayetoka naye usiku wa uzinduzi wa filamu yake mpya Road to Heaven.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amendika ujumbe wa kumtafuta mtu huyo atakayekuwa naye usiku huo, kwani akisema raha ya tukio kama hilo lazima uwe na mtu pembeni yako, kwani anatarajia kuvunja kabati kwa kupendeza, lakini haitakuwa na maana kama atakuwa peke yake.
Kupitia akaunti yake Instagram Wema ameandika ” Bado siku 4 tu, nilisema kuna tatizo, kupendeza nitapendeza tena sana tu ila sasa sina date wa kwenda naye raha ya zulia jekundu uwe na mtu… nani atajitolea kuwa mtu wangu kwa usiku huo wa kukumbukwa!?”..
Mwisho wa wiki hii Wema Sepetu anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayotwa ‘Road to heaven’ aliigiza na wasanii wengie wakali wa filamu.