Baada ya mahakama kuu kumuhukumu Lulu miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia, hatimaye muigizaji mwenzake Wema Sepetu amempa pole kufuatia hukumu hiyo iliyotolewa leo.
Wema amempa pole hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya hukumu kutolewa na mahakama kuu kanda maalumu ya Dar es Salaam.
Lulu amehukumiwa leo katika mahakama kuu kanda maalum ya Dar es Salaam baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia dhidi ya aliyekuwa muigizaji nyota wa Bongo Movie, Steven Kanumba.