Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Wakazi amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kutoa maagizo kwa Wizara ya michezo na Basata kuvunja uongozi wa shirikisho la muziki nchini.
Kupitia kwenye akaunti yake Instagram ameandika”Heshima yako @samia_suluhu_hassan (MAMA SAMIA) naomba utoe maagizo kwa Wizara (kupitia Waziri Mchengerwa na Katibu Mkuu Dr Abbasi) waiambie BASATA kuvunja uongozi wa Shirikisho La Muziki!
Hawajui Majukumu yao na pia Wanatugawa Wasanii kutokana na itikadi za kisiasa! Wamepoteza Sifa za uongozi!
Huyu ni @addonovember Rais wa Shirikisho la Muziki, anasema amemteua Steve Nyerere awe Daraja la Shirikisho na Serikali, wakati wao Shirikisho ndio daraja lenyewe.
Ila kibaya zaidi anasema sisi tunaopinga uteuzi ni wanaharakati tu wa vyama vya upinzani. Pia Shirikisho linasimama upande wa Chama cha Mama Samia (CCM) na wao wapo kulinda maslahi na matakwa ya Serikali na sio ya wasanii.
Kwa Kauli hizo ni dhahiri kuwa amepoteza Sifa za Uongozi, na Sisi wasanii ambao tunamini katika amani, demokrasia na kutofautisha siasa na taasisi za umma na tasnia, tumehuzunishwa na kauli hizo na tumepoteza imani na uongozi wake (achilia mbali swala la Steve Mengele) na tunataka Uongozi huo uvunjwe ili tufanye Uchaguzi upyaaa! Nimeongea kama Msanii, ila pia kama msemaji wa Kisekta wa ACT Wazalendo. Viongozi wame onyesha incompetence & self serving attitude, they must go.
Natanguliza Shukurani.
The Leader.