Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki amefunguka ya moyoni kuhusu baadhi ya madaktari kutaka wajawazito wanaokwenda kujifungua wafanyiwe upasuaji badala ya kujifungua kwa njia ya kawaida kwa kisingizio cha njia ndogo ya mtoto kupita.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Roma ambaye ni baba wa watoto wawili na mume wa mke mmoja ameandika ujumbe mzito.
“Hospitali nyingi tunapowapelekaga wake zetu na wachumba zetu na dada na mama na shangazi na rafiki zetu wa kike ili wakajifungue, mara nyingi utakuta madaktari mnatengeneza mazingira ili tu wenza wetu hawa wajifungue kwa njia ya operation!! kwa maana gharama yake ni kubwa kuliko njia ya kawaida.
“Hata kama mtu anauwezo wa kupush kwa njia ya kawaida, mtasema tu njia yake ya uzazi ni ndogo, hii kauli imekuwa kawaida kwa wajawazito wengi sikuhizi!! mara atawekewa dripu la uchungu na lisi-function, ili mradi tu tu-sign ile karatasi mtu apigwe kisu.
Mnawaweka vilema, alama na makovu wachumba zetu kwa maslahi yenu binafsi! Inatuumiza sana sisi waume zao, hata na wao, ingawa wanakuwa hawana jinsi wala maamuzi kutokana na hofu.
Anyways, sio hospitali zote na sio madaktari wote, ila tunao wengi tu wanaotenda hayo na tunaishi nao na tunashuhudia hayo!!narudia tena sio wote,ila wapo baadhi waliokosa weledi katika field yao hii.
Nakubali operation ni nzuri na salama, lakini ifanyike inapobidi, isiwe kwa maslahi hasa ya pesa, mishahara najua haitoshi, lakini hata sisi tunatafuta kwa shida sana, so tusiwape vidonda mama zetu.
Nawapenda dada zangu wote na naelewa maumivu yenu!! mungu awape uzao ulio mwema na salama amina inshallah asalam aleykum.