Baada ya Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Professor Jay) amesema kuwa mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi (Sugu) amewataka wananchi wasiogope na yeye kukamatwa badala yake wapaze sauti.

Kauli hiyo ya Profesa Jay imekuja baada ya kwenda Mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.

Professor Jay amesema kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo ambapo RCO na RPC wa Mbeya watasimama kutoa ushahidi wao.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Profesa Jay ameandika “SUGU kaniambia niwaambie ‘MSIOGOPE’ bali endeleeni kupaza Sauti!!Kesi yao inaendelea leo saa Tatu asubuhi hii katika mahakama kuu ya Mbeya, ambapo RCO na RPC wa Mbeya watasimama kutoa ushahidi wao LEO,”.

Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli ambapo wanadaiwa kuitoa Disemba 30 mwaa jana kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge mkoani Mbeya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *