Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari mmoja kuchomoa bastola na kumuoneshea aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye mbele ya wahandishi.

Nchemba kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema kitendo hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika atahadhibiwa.

Amesema amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumska mhusika.

Askari akimuoneshea bastola Nape Nnauye jana
Askari akimuoneshea bastola Nape Nnauye jana

Aliyoandika Mwigulu Nchemba “Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini,”.

Aliongeza “Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *