Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maua Sama amedai kuwa mbali na kuwa alijua Nay wa Mitego ni mwenye masimango lakini hakujua kama msanii huyo ni mwenye “mdomo kupitiliza” .

Maua aliutumia ukurasa wake wa instagram ikiwa ni siku chache tangu aachie wimbo aliomshirikisha Nay wa Mitego uitwao ‘Baba Jeni’ . Wimbo huo umetayarishwa na Bin Laden.

“Nilikua najua  Nay wa Mitego ana Masimango lakini nlikuwa sijui kama ana Mdomo kupitiliza Aliandika Maua Sama.

Hata hivyo ilihisiwa kuwa pengine Maua hakuwahi kulijua hilo kwa mujibu wa uandishi wa Nay kwenye wimbo wake huo ambao uliandikwa kwa ufundi wa kupokezana ushairi juu ya kuhusiana na wazo lao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *