Muigizaji Irene Uwoya amemshukuru Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuwathamini na kuwaamini wanawake kwa kuwapa nafasi za juu katika kuongoza taifa la Tanzania.
Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa hawezi kumsahau Rais huyo kutokana na uamuzi wake wa kutoa nafasi kubwa kwa wanawake katika serikali yake, zikiwemo nafasi za uwaziri, majaji na hata Spika wa bunge, na kwamba, Rais huyo ndiye aliyempa motisha ya kugombea ubunge.
Uwoya meandika “Namshukuru sana Rais mstaafu… Mh. JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa kutupa wanawake heshima na kututhamini… Alitupa nafasi nyingi sana katika nafasi za mawaziri, majaji na spika…
Pia ameongeza ”Na hata mimi kama msanii nilihamasika na kuona naweza kugombea ubunge… Kiukweli amefungua njia na ameweka mwanga mkubwa kwa viongozi wengine na wao wakaendelea kuthamini na kuheshimu mchango wetu katika jamii ndiyo maana hata tukapata makamu wa Rais mwanamke kwa mara ya kwanza Tanzania”.
Muigizaji huyo amesema hayo kwenye siku ya Wanawake Dunia ambayo imeadhimishwa jana dunia kote.