Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kupitia akaunti yake ya Twitter amesema kuwa hawezi kujibishana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwenye mitandao.
Hayo yamejiri baada ya Gwajima kumtaka Halima Mdee kumuomba radhi Spika wa Bunge Job Ndugai kwa maelezo kuwa alimtukana wakati wakiwa Bungeni.
Halima Mdee kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika kuhusu kinachoendelea kati yake na Spika Ndugai baada ya kutakiwa kufika kamati ya maadili ya Bunge kwa ajili ya mahojiano.
Mbunge huyo ameandika ’Namuheshimu sana Mch. Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.
Pia ameongeza kwa kuandika “Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO”.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema), juzi wamehojiwa na Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kwa muda wa saa mbili – saa moja kila mmoja.