Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa albamu yake ‘Money Mondays’ imeingiza milioni 40 za mauzo kwa mwezi mmoja toka iingie sokoni.
Vanessa Mdee amesema mpaka sasa ameuza nakala zaidi ya elfu 4 na kila nakala moja anaiuza kwa shilingi elfu 10 ambapo kwa mahesabu ya haraka haraka ameingiza zaidi ya shilingi milioni 40 ndani ya mwezi mmoja.
Mwanamuziki huyo amebainisha hayo kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kuwashukuru mashabiki wake kwa kuipokea albamu hiyo.
Ameanza kwa kuandika “Namshukuru Mungu tumeshauza nakala zaidi ya elfu nne za CD ya #MoneyMondaysTheAlbum kwa sasa tupo Zanzibar kuendelea na mauzo. Asanteni Sana kwa support yenu. Let’s get to 10,000 copies in less than a month. Usinunue CD ya #moneymondays isiyokuwa na sticker ya TRA.
Hii ni albamu ya kwanza ya mwanamuziki huyo toka aanze muziki ambapo ameiachia mapema mwaka huu.