Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz leo anatarajia kuzindua albam yake ya pili ijulikanayo kama ‘A Boy From Tandale’.
Uzinduzi wa albam hiyo unafanyika leo nchini Kenya ambapo team nzima ya WCB ipo jijini Nairobi kwa ajili ya uzinduzi wa albam hiyo ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo 14 ambapo nyingine amefanya na wasanii wenzake.
Albam hiyo ya Diamond ni ya pili kuachiwa ambapo baada ya kuzinduliwa nyimbo zake zitaanza kusikika sehemu tofauti.
Diamond amewataka wakazi wa jiji la Nairobi na vinga vyake kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumpa sapoti katika uzinduzi huo.
Kwa upande wa mmoja wa mameneja wa mwanamuziki huyo, Mkubwa Fella amesema kuwa wameamua kufanyia uzinduzi nchini Kenya kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Kenya na Tanzania.