Akaunti ya YouTube ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz imerejea baada ya kuripotiwa kuchukuliwa na wadukuzi jambo ambalo lilisababisha kusimamishwa kwake.

Chaneli ya Diamond Platnumz, ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 6.5 na yenye kutazamwa na watu zaidi ya bilioni moja, ilisemekana kuwa ilidukuliwa siku ya Jumapili.

Afisa wa kampuni ya rekodi ya Diamond Platnumz, Wasafi, alisema kuwa walipokea barua pepe kutoka YouTube ikiwajulisha kuwa akaunti hiyo imesimamishwa.

Majid Ramadhani alisema ilisitishwa baada ya wadukuzi hao kuweka wazi maudhui ambayo yalikiuka miongozo ya jukwaa la kidigitali.

Amesema kwamba walipata hasara kubwa na wanajitahidi kusuluhisha suala hilo.Siku ya Jumatatu, nyota huyo wa muziki aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha kuwa ukurasa huo umerejea.

Chaneli hiyo ina wafuasi zaidi ya milioni 6 na kumfanya Diamond kuwa kati ya wasanii wenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Youtube barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *