Watu wawili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Sharon kupindika katika eneo la Mabanzini milayani Babati.
Basi hilo lilikuwa linatoka mkoani Dodoma kwenda Arusha limepinduka eneo la mabanzini mjini Babati na kusababisha vifo vya watu hao wawili.
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali ya Mrara mjini Babati mkoani Manyara kwa ajali ya matibabu kutokana na majeraha waliyoyapata kwenye ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusababishwa vifo vya watu wawili ambao ni kondakta wa basi hilo pamoja na mtoto mdogo.