Mgombea, Ahmad Ahmad kutoka nchini Madagascar ameshinda nafasi ya urais wa CAF kwenye uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo barani Afrika uliofanyika leo nchini Ethiopia.

Mgombea huyo ameibuka mshindi baada ya kumshinda rais wa sasa wa Shirikisho hilo Issa Hayatou kutoka nchini Cameroon.

Katika uchaguzi huo Ahmad ameshinda kwa jumla ya kura 34 dhidi ya kura 20 alizopata Issa Hayatou.

Hayatou amekua rais wa Shirikiksho hilo kuanzia Machi 10 mwaka 1988 akidumu miaka 29 kama rais wa Shirikisho hilo barani Afrika.

Ahmad Ahmad alikuwa akiungwa mkono na nchini wanachama wa COSAFA na CECAFA ambao walimthibitishia kumpigia kura huku Issa Hayatou akitegemea kura upande wa Afrika Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *