Muigizaji wa Bongo Movie, Agness Suleiman kwa mara ya kwanza amefunguka madai ya kuhusishwa kimapenzi na aliyewahi kuwa mume wa msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ Ashraf Uchebe kuwa ilikuwa ni kiki.
Agness alisema kuwa Uchebe alimtafuta na kumuomba wafanye kiki hiyo ili kumuumiza roho zilipendwa wake Shilole.
Amesema “Uchebe aliniomba sana, aliwahi kunipigia simu zaidi ya mara mbili akaniambia anataka afanye kitu ili amuumize Shilole kwa sababu hata yeye alimuumiza sana.
Pia amesema kuwa “Nilikataa kwa sababu niliona sio kitu kizuri lakini baada ya kuniomba sana ndio nikakubali kufanya ile kiki, ila kiukweli sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Uchebe.
Wawili hao walihusishwa kutoka kimapenzi baada ya picha zao za mahaba kusambaa mitandao ikiwa ni siku chache baada ya Shilole kuachana na Uchebe.