Raia wa Afrika Kusini wameanza kupiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkubwa kuwahi kufanyika nchini humo tangu kuisha kwa ubaguzi wa rangi 1994.

Takriban watu 250,000 ambao wanafuzu kupiga kura watashiriki uchaguzi huo wa serikali za mitaa .

Wapiga kura hao ni wajawazito,walemavu na wale wataokaokuwa mbali na maeneo yao ya kupiga kura siku ya Jumatano,ambayo ndio siku ya shughuli hiyo.

Tume ya kupiga kura IEC imesema kuwa ina matumaini kwamba uchaguzi huo utakuwa huru,usio na mapendeleo licha ya hali mbaya ya hewa wakati wa kampeni.

Mwenyekiti wa tume hiyo IEC Glen Mashinini pia alipiga kura.

Amewataka raia wa Afrika Kusini kupiga kura kwa amani.

Chama tawala cha ANC kinakabiliwa na upinzani mkali tangu kichukue madaraka 1994 katika mji wa Johannesburg,Tshwane ikiwemo mji mkuu wa Pretoria na Nelson Mandela Bay.

Vyama viwili vya upinzani Demokratic Alliance na Economic Freedom Fighter pia vinapanga kudhibiti mabaraza hayo matatu lakini ANC kina matumaini ya kushinda katika maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *