Waziri wa afya wa jimbo la KwaZulu Natal, Sibongiseni Dhlomo ameingia kwenye rekodi maalum baada ya kusitisha shughuli za kiserikali ili kuifanyia uchunguzi miili ya marehemu waliokuwa kwenye hospitali kuu ya jimbo hilo.
Hatua hiyo ilifuatia kitendo cha watumishi wa chumba cha kuhifadhia maiti kutotokea kazini kwa madai ya kuwa wagonjwa.
Sibongiseni Dhlomo, ambaye ni mtaalamu wa Forensic Pathology, alilazimika kukatisha ratiba zake na kuingia kwenye mochwari ya Park Rynie kuifanyia uchunguzi uchunguzi wa baada ya vifo miili mingi iliyokuwa kwenye chumba hicho.
Waziri huyo na timu yake wanatarajiwa kukamilisha uchunguzi wa miili 17 ndani ya siku 2 huku msemaji wa kituo cha Desmond Motha akiwahakikishia ndugu waliokuwa wakisubiri kuzika miili ya ndugu zao mwishoni mwa wiki kuwa wataipata ndani ya wakati.
Taarifa rasmi ya kituo hicho cha afya imemnukuu waziri huyo akiwahakikishia wananchi hao upatikanaji wa miili hiyo kufikia Jumapili.