Raia wa Afrika Kusini wameanza kufukuza raia wa kigeni waliopo nchini humo wengi wao wakiwa ni wanigeria.
Vyombo vya habari nchini Nigeria vimekuwa vikiripo kuwa raia 97 wa Nigeria wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu tofauti walifukuzwa kutoka Afrika Kusini siku ya Jumatatu.
Msemaji wa wizara hiyi Mayihlome Tshwete amesema kuwa mamia ya watu wasio na vibali walisafirishwa kutoka nchini humo, wengi wao kutoka na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC.
Wengine ni raia wa Pakistan, China, Bangladesh na Somalia nao wamefukuza ndani ya nchi hiyo kutokana na sababu mbali mbali.
Afrika Kusini imekumbwa na ghasia dhidi ya raia wa kigeni na visa vya kuporwa kwa maduka yanayomilikiwa na wahamiaji.
Afrika Kusini huwafukuza karibu watu 30,000 kila mwaka kutokana na machafuko ndani ya nchi hiyo.