Mwanamuziki wa Bongo fleva, Afande Sele amefunguka na kuwachana baadhi ya viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo kutokana na viongozi hao kukosa msimamo thabiti katika baadhi ya mambo.

Afande Sele ametumia ukurasa wake wa Facebook kufikisha ujumbe wake kwa watanzania huku akisema anashindwa kuwaelewa viongozi wake wanasimamia jambo gani kiasi cha wao kama wanachama wanashindwa kukielewa chama hicho kama ni malaika au shetani.

Afande Sele ameandika ‘Chama changu cha Act-Wazalendo bwana wakati flani hata mimi sikielewi kama ni malaika au shetani. Ni kama kiumbe aitwae mkunga haeleweki ni samaki au nyoka zaidi tumekuwa kama popo hatupo katika kundi la ndege au mnyama…labda hatueleweki au hatujielewi kwa mfano wakati wa kampeni viongozi wetu walijikita kuponda wapinzani wenzetu hasa mzee Lowasa na UKAWA na baada ya uchaguzi viongozi wetu wakampongeza Magufuli kiasi cha kujipendekeza hadi wakampa Ilani ya chama chetu akaitumie akiwa Ikulu. sasa ajabu leo hii tumegeuka tena kwa kiongozi mkuu kila siku anamponda Rais Magufuli na chama chake halafu kiongozi wangu mwingine comrade mchange yeye kila siku anamponda mzee Lowasa na ukawa yake’.

Mbali na hilo Afande Sele anazidi kushangaa kuona viongozi wake sasa hivi katika mgogoro wa Chama Cha Wananchi CUF wote wamegeuka na kumpa support Profesa Ibrahim Lipumba kiasi cha wao kama wanachama wanashindwa kuelewa wasimamie wapi.

Pia aliongeza kwa kuandika “Katika mgogoro wa CUF unaoendelea sasa hivi eti viongozi wote hao wa chama chetu wamejigeuza team Lipumba…sasa sielewi sisi kama wanachama tusimamie wapi….’Nyuma ya pazia’dilidilisha…mchongo=mchongoma…ni bora kuwa Moto au Baridi kuliko kuwa vuguvugu kwani vuguvugu ni ishara ya unafki ambao hata maandiko yanakataza…Kweli itatuweka huru”.

Afande Sele  aligombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Morogoro mjini kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa tiketi ya chama hicho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *