Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Afande Sele amedai kuwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa marufuku.
Afande Sele ni mwanasiasa na aligombea ubunge katika jimbo la Morogoro mjini kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo katika uchaguzi mkuu uliyopita.
Mwanamuziki huyo amedai yupo mikononi mwa polisi toka jana ambapo anashikiliwa kutokana na kushawishi wananchi wa mkoa huyo kushiriki maandano yaliyopigwa marufuku maarufu kama UKUTA.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Afande Sele ameandika “Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya Msamvu.
Pia Afande Sele kupitia ukarasa wake huo aliongeza kwa kuandika “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”.
Afande Sele ni miongoni mwa wasanii wakongwe hapa nchini ambaye amewahi kutamba miaka ya nyuma na nyimbo zake kama Darubini Kali, Dunia Inamambo na Waache Wapige Wayowe na nyingine kibao.
Kwasasa msanii huyo ameamua kujikita katika siasa kama walivyofanya wasanii wenzake Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ambao kwasasa ni wabunge.