Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’ ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa kwa kuwaunganisha Watanzania katika maendeleo ya taifa hususan vijana bila kujali tofauti za kiitikadi.
Ametoa pongezi hizo mbele ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan Msamvu mjini Morogoro.
Makamu wa Rais alisimama kwa muda kuzungumza na wananchi alipokuwa njiani kwenda mkoani Dodoma.
Afande Sele amesifu uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa uchapakazi na uwajibikaji kwa wananchi na kuweza kuwaunganisha Watanzania katika suala la maendeleo pasipo kujali itikadi zao.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi nzuri ya kuwaunganisha Watanzania kama walivyofanya waasisi wa Taifa letu hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja Abeid Amaan Karume. “
Afande Sele hakuweza kuzungumzia masuala ya kiasa, tofauti na walivyotarajia baadhi ya mamia ya wananchi waliokuwa wamejitokeza eneo la Msamvu na baada ya kuitwa na Makamu wa Rais, umati wa wananchi ulimshangilia kwa kulitamka jina lake la Afande Sele.
Afande Sele ambaye aliwahi kutamba na kibao chake cha ‘Mkuki Moyoni’ pamoja na ‘Darubini Kali’ alishiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2015 akiwania Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kupitia tiketi ya Chama cha ACT- Wazalendo, lakini alishindwa.
Mwanamuziki huyo wiki chache zilizopita aliwamwagia lawama viongozi wa chama chake cha ACT- Wazalendo kuwa kusema kuwa viongozi wa chama hicho hawana dira zaidi ya kuiponda Serikali ya awamu ya tano.