Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow amepewa hifadhi nchini Senegal kutokana na mzozo uliopo nchini mwake bada ya rais wa sasa wa Gambia Yahya Jammeh kupinga matokeo ya uchaguzi.

Shirika la habari nchini Senegal linasema kuwa rais wa nchi hiyo Macky Sall, amekubali kumpa hifadhi Barrow kwenye mji mkuu Dakar hadi pale atakapoapishwa tarehe 19 mwezi huu.

Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba.

Siku ya Jumamosi rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita alimtaka rais wa Gambia kuondoka madarakani ili kuzuia kuzuia umwagaji damu.

Alikuwa akizungumza wakati wa mkutano Afrika na Ufaransa kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako, ambao ulitawaliwa na mzozo ulio nchini Gambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *