Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto amesema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na ufisadi na kujenga uwajibikaji.
Zitto amesema kuwa wanaamini kwamba kuheshimu, kulinda demokrasia na kuzingatia utawala wa sheria ndiyo msingi wa mapambano dhidi ya ufisadi.
Zitto amesema kuwa pamoja na changamoto zinazoendelea kutokea, wataendelea kutoa mapendekezo katika kutatua changamoto hizo kabla na baada ya kuunda serikali.
Amesema tafiti zinaonesha kuwa demokrasia na kuzingatiwa utawala wa sheria na haki za binadamu ndiyo msingi wa maendeleo kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa.
Hata hivyo, alisisitiza kwamba vita dhidi ya rushwa na ufisadi lazima ifanywe kwa kuzingatia misingi ya haki, utu na usawa.
Kutokana na hali hiyo, alimuomba Rais Magufuli na serikali yake kuhakikisha kwamba watumishi wote wa umma 134 waliosimamishwa kazi hadi kufikia Agosti mwaka huu, kufikishwa katika vyombo husika vya kinidhamu na sheria ili ukweli kuhusu tuhuma zao ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe.