Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibrah kutoka Konde Gang Worldwide amepata pigo baada ya akaunti yake ya YouTube kufutwa kwenye mtandao huo licha ya kuwepo kwa nyimbo zake.

Ukiingia kwenye akaunti hiyo kupitia link iliyopo kwenye BIO yake ambayo ameweka video ya wimbo wa Notachelewa utakutana na ujumbe usemao “This video is no longer available because the YouTube account associated with this video has been terminated.”

Kwa mujibu wa YouTube, akaunti kuwa terminated kunaambatana na sababu kadhaa ikiwemo kurudia makosa mara kwa mara ya kukiuka miongozo ya jamii iliyowekwa au masharti ya huduma kwenye maudhui yako kama yenye kuashiria uvunjifu wa amani, unyanyasaji, chuki,

Mengine ni ponografia na zingine za mlengo mbaya. Pia zingine hufutwa kutokana na masuala ya hakimiliki (Copyright termination)

Akaunti ikiwa terminated mtumiaji hataweza kuitumia tena, kuimiliki au kutengeneza nyingine kwa taarifa za awali. Akaunti ikiwa terminated mmiliki hupokea barua pepe ikielezea sababu zilizopelekea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *