Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imesema kuwa haina uwezo wa kulipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.

Akiongea jana  Oktoba 20, 2017 kwa njia ya simu na chombo cha habari cha Kimataifa cha Uingereza (Reuters) Afisa wa Fedha wa Acacia, Andrew Wray kampuni hiyo haina uwezo wa kulipa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania.

Washirika wakubwa wa Acacia, Barrick Gold siku ya juzi Oktoba 19 walikubalina na serikali ya Tanzania kuwa watalipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Tanzania pamoja na kugawana mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *