Abiria wa mabasi ya mwendokasi wamefanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuandamana kwenye njia ya mwendokasi katika kituo cha Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam.
Vurugu hizo zilisababishwa na uhaba wa magari hayo ya mwendokasi ambapo abiri hao waliyasubilia kwa muda mrefu.
Magari yote yaliyokuwa yanapita kituoni hapo yalikuwa yamejaa kiasi cha kutoweza kuchukua abiria wengine kwenye kituo hicho.
Baada ya changamoto hiyo kudumu kwa saa kadhaa ndipo abiria walipoanza kupita kwenye njia ya mwendokasi kwa kuandamana wakishinikiza magari yaongezwe ili kutatua changamoto hiyo.
Hata hivyo baada ya muda changamoto hiyo ilitatuliwa kwa magari ya Express kuanza kuchukua abiria kituoni hapo na hatimaye shughuli nyingine katika eneo hilo kuendelea kama kawaida.