Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemsimamisha kuendelea na masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul Nondo baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), amesimamishwa kwa barua iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye.

Profesa Anangisye amesema mwanafunzi anapokuwa amepandishwa kizimbani na akawa na kesi ya kujibu husimamishwa na akishamaliza kesi yake anarejea kuendelea na masomo.

Pia taarifa hiyo imesema kuwa mwanafunzi huyo atarudi chuo mpaka kesi yake itakapomaliza na kutolewa hukumu.

Abdul Nondo jana aliachiwa kwa dhamana ambapo anakabiliwa na makosa ya kusambaza taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiojulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *