Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa usiku wa kuamkia leo  kwenda mkoani Iringa kwa ajili ya kujibu.

Taarifa zilizotolewa na wakili wake, Jebra Kambole leo zinaeleza kuwa sasa hivi Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kujibu mashtaka.

Mnamo Machi 6, 2018 Abdul Nondo alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kupatikana siku iliyofuata Machi 6, 2018 mjini Mafinga, mkoani Iringa ambako alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kabla ya kurejeshwa Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo, tangu akamatwe, Abdul Nondo hajawahi kuzungumza na wakili wake wala vyombo vya habari jambo ambalo limekuwa likipingwa na watetezi wa haki za binadamu.

Leo Machi 21, 2018 Mwanasheria wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Paul Kisabo amewasilisha shauri la maombi Mahakama Kuu kutaka DPP, DCI, IGP wajibu mashtaka kwanini hawajampeleka Abdul Nondo Mahakamani na wamemshikiria kinyume na sheria mpaka sasa hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *