Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdukiba amekanusha kuwa wimbo wake mpya ‘Jeraha’ amemuimbia video vixen Bongo, Tunda.

Habari zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Abdukiba amechanganywa kimapenzi na kuumizwa baada ya kuachwa na Tunda kiasi cha kumuandikia wimbo huo.

Mwanamuziki huyo ambaye ni mdogo wake Alikiba amesema kuwa wimbo huo yeye hajamuimbia Tunda kama ambavyo watu wanadai au wanahisi bali ni hisia tu na aliuandika wimbo huo kupitia mambo mbalimbali ambayo hata yeye aliyapitia na kuamini kuwa watu wengine wameyapitia ila hakumuandikia mrembo Tunda kama watu wasemavyo.

Wimbo huo ameuachia wiki hii ambao unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na kugusa nyoyo za mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *