Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdu Kiba amefunguka na kusema kuwa hana tofauti na msanii mwenzake Mbosso licha ya kuwa lebo tofauti za muziki.

Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa Alikiba amesema kuwa hana shida yoyote na Mbosso kwa kuwa walikuwa marafiki muda mrefu toka Mbosso yupo Yamoto Band hiyo hawana tofauti isipokuwa ni maneno ya mashabiki tu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa Collabo yake na Mbosso itaushangaza ulimwengu siku wakiamua kufanya ngoma ya pamoja kwa yeye na Mbosso hawana tatizo na ni rafiki yake wa muda.

Pia Abdukiba ameongeza kuwa mara nyingi wanakutanaga kwa Prouducer Mocco na wasanii wenzake huwaangalia na kusubiri kitu gani kitatokea lakini mwisho wa siku hupiga stori na kucheka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *