Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana amezindua albam yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘A Boy From Tandale’.
Uzinduzi wa albam hiyo umefanyika katika jiji la Nairobi nchini Kenya ambapo team nzima ya WCB ilikuwepo kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa albam ya mwanamuziki huyo.
Mbali na team ya WCB pia mwanamuziki wa Marekani, Omarion alikuwa kwa ajili ya kutoa sapoti katika uzinduzi wa albam hiyo.
Mameneja wafunguka kuhusu albam kuzinduliwa Kenya.
Meneja Diamond, Babu Tale amesema kuwa wameamua kufanyia uzinduzi nchini Kenya kwasababu Kenya ni makao makuu ya msauala ya biashara Afrika Mashabiki kutokana na kuwa na makampuni hivyo wakaamua kutumia fursa hiyo ili kuitangaza albamu hiyo.
Kwa upande wa Mkubwa Fella amesema kuwa wameamua kufanyia uzinduzi nchini Kenya ili kuimarisha ushirikiano uliopo miongoni mwa nchi hizi mbili.