Shirikisho la soka barani Afrika Caf limeongeza kitita cha fedha zinazozawadiwa washindi katika michuano yote kuanzia mwaka 2017 kueleka 2020.

Washindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika watapata dola milioni 4,wakati ambapo Ivory Coast ilizawadiwa dola milioni 1.5 iliposhinda taji hilo mwaka 2015.

Mshindi wa kombe la vilabu bingwa Afrika atajishindia dola milioni 2.5 badala ya dola milioni 1.5 ambazo Mamelodi Sundowns walijishindia mwezi uliopita.

Wakati huohuo fedha za mshindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika upande wa wanawake zitaongezwa na kufikia 80,000 mwaka 2019 kutoka dola 50,000 mwaka huu.

Fedha hizo ni chache mno ikilinganishwa na zile inazopewa timu iliomaliza ya mwisho katika kombe la bara Afrika upande wa wanaume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *