Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametetea hatua ya nchi yake na kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini.
Rais Kenyatta amesema kuwa Kenya imejitolea katika kuchangia amani katika kanda hii na dunia nzima lakini akaongeza kuwa heshima ya nchi haiwezi kuchafuliwa.
Kenyatta amezungumza hayo wakati akiongoza hafla ya kufuzu kwa wanajeshi kwenye chuo cha kutoa mafunzo ya kijeshi cha Lanet kaunti ya Nakuru.
Amesema kuwa uamuzi wa kuondoka kwenye mpango huo wa amani, unafuatia visa vinavyaokua ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, ambapo Umoja wa Mataifa ulimlaumu kamada kutoka nchini Kenya.
Kenyatta ameongeza pia kuwa Kenya ina mpamgo ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka ujumbe huo ambao alisema umeanza kuwalaumu wakenya.
Kenyatta amesema kuwa kenya imachangia makanda wenye tajriba ya juu katika masuala ya kulinda amani wakiwemo Luteni Jenerali Daniel Opande ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha kulinda amanai nchini Sierra Leone na Luteni Jenerali Ngondi ambaye alikuwa kamanda nchini Liberia miongoni mwa wengine.