Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imewataka watoa huduma za afya na wafanyabiashara za dawa nchini  kuzirudisha TFDA dawa za Malaria  pamoja na dawa za Vijiuasumu (Antibiotic) zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17 zilizobainika kuwa ni bandia.

Dawa hizo zilibainika kuwa bandia kutokana na zoezi la ukaguzi lililofanywa na mamlaka hiyo.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo ametaja baadhi ya  dawa hizo kuwa  ni vidonge vya aina ya Eloquine, Quinine Sulphate 300mg ambazo hutibu Malaria, Erythromicin, Doxycyline 100mg na Siproflaxine  ambazo hutumika kama Viuajisumu zilizokamatwa katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Mara, Geita na Shinyanga.

 

Amesema uchunguzi wa awali umeonesha kwamba dawa hizo bandia zinatengenezwa hapa nchini katika makazi ya watu na maeneo mengine ya kificho ambapo dawa zilizoisha muda wa matumizi pia huongezwa muda kwa kuondoa alama za zamani na kubandika mpya na kishwa kuuzwa madukani kwa wagonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *