Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema kitendo kinachofanywa na walimu cha kuwarekodi wanafunzi wanapofanya makosa na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii ni kinyume cha maadili ya kazi yao.

Amesema mwalimu ni kiongozi katika kutunza nidhamu ya mwanafunzi kwa kipindi chote awapo shuleni na hapaswi kumrekodi mwanafunzi na kusambaza video ikionesha mwanafunzi ana makosa.

“Nashangaa ninaposikia matukio hayo, sio vyema na hairuhusiwi kabisa kwa mwalimu kufanya tukio kama hili, mwalimu anapaswa kuwa kiongozi na mlinzi wa nidhamu kwa wanafunzi,” alisema Jafo alipozungumza na gazeti hili hivi karibuni.

Amesema mwalimu yeyote aliyehusika kurekodi video hizo na kutuma katika mitandao mbalimbali ya kijamii anapaswa kutambua kuwa, kitendo anachokifanya ni kinyume cha maadili ya kazi yake na kwamba mwanafunzi anapokosea anapaswa kupewa adhabu kulingana na sheria inavyotaka na sio kutuma video katika mitandao kwani sio adhabu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *