Maafisa wa kampeni wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump wamekiri kwamba mgombea huyo yupo nyuma ya mpinzani wake Hillary Clinton.

Bw Trump ameonekana kukiri uwezekano kwamba anaweza kushindwa uchaguzi huo mkuu nchini Marekani.

Trump amesema iwapo atashinda, ashindwe au atoshane nguvu na mpinzani wake, ataridhishwa na juhudi zake.

Siku moja baadaye, alitangaza hatua ambazo atazichukua siku 100 akiwa uongozini iwapo atashinda.

Miongoni mwa hizo ni kuweka masharti mapya kwenye mchakato wa kisiasa wa kutafuta uungwaji mkono kisiasa, mikataba ya kibiashara na mabadiliko ya tabia nchi.

Kura mpya za maoni zinaonesha Bi Clinton yupo mbele sana kitaifa na katika majimbo mengi yanayoshindaniwa.

Maafisa wake kampeni wa Clinton wamebashiri kwamba huu utakuwa uchaguzi mkubwa zaidi katika historia ya Marekani.

Meneja wake wa kampeni Robbie Mook amesema watu watajitokeza kupiga kura zaidi ya wakati wowote awali.

Kura za maoni katika majimbo ambayo ni ngome ya chama cha Republican kwa mfano Utah na Arizona zinaonyesha huenda majimbo kwa mara ya kwanza katika miongo mingi akaunga mkono mgombea wa Democratic.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *