Zaidi ya nyumba 150 za wakazi wa Tegeta A Kata ya Goba jijini Dar es Salaam zimebomolewa kwa madai ya kujengwa eneo ambalo sio lao huku Kaya zaidi ya 450 zikikosa makazi ya kuishi.

Ubomojai huo umepingwa na wananchi hao wakidai eneo hilo ni lao na wapo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Zoezi la ubomoaji wa nyumba hizo lilisimamiwa na askari polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku wakiwa katika magari yenye namba PT, 3475, 1986 na  3675 huko kukiwa na askari hao zaidi ya 15.

Mmoja wa wananchi hao, Macarios Turuka  amesema eneo hilo kwa kipindi kirefu lilikuwa halitumiki na lilikuwa ni vichaka vya wahalifu kwani wanawake walikuwa wakibakwa na kutumiwa na watu kwa uhalifu ndipo walipoingia na kujenga.

Amesem kuwa baada ya kuanza ujenzi ndipo alipo ibuka Benjamini Mutabagwa na kueleza kuwa ni lake ndipo walipofungua kesi mahakama ya Kimara ambapo alishindwa kupeleka vielelezo vya umiliki wa eneo hilo.

Mwanasheria anayewatetea wananchi hao, Moses Chunga amesema kitengo cha kubomoa nyumba hizo ni kukiuka sheria za mahakama kwani kuna kesi ya msingi namba 188/ 2016 waliyofungua mahakama kuu ya ardhi ambapo walitakiwa tarehe 31 mwezi huu kwenda kuisikiliza lakini wanashangaa kuona nyumba hizo zikibomolewa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela amesema kampuni yake imevunja nyumba hizo kwa amri ya mahakama na polisi walikuwepo kusimamia zoezi hilo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *