Shirika la ndege la Etihad limepokea hati ya uthibitisho wa kuwa na hadhi ya nyota tano, kutoka kwa taasisi ya Skytrax ambayo inajihusisha na utafiti wa ubora wa huduma za anga Uingereza.
Hadhi hiyo inatokana na ukaguzi wa huduma za anga uliofanyika kwa miezi mitatu.
Etihad imetangazwa kutunukiwa hadhi hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Uvumbuzi kinachomilikiwa na shirika hilo mjini Abudhabi.
Hadhi ya Nyota tano kwa mashirika ya ndege hutolewa na Skytrax ili kuthibitisha ubora wa juu katika huduma za anga kwa mashirika mbalimbali.
Vigezo vinavyozingatiwa katika utoaji wa hadhi hiyo ni pamoja na mpangilio wa ukaaji kwa abiria, usafi ndani ya ndege, burudani na huduma ya chakula.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Etihad, Peter Baumgartner amesema, “Hadhi hii ni ishara ya matunda ya juhudi zetu za siku nyingi katika ukuaji wa huduma zetu za anga. Shirika letu limekuwa likizikabiri changamoto zinazojitokeza katika huduma za anga kwa kuboresha huduma ili kulifanya kuwa mfano wa kuigwa duniani kote.