Donald Trump na Hilary Clinton ambao ni wagombea urais nchini Marekani wamechuana tena katika awamu ya tatu na ya mwisho ya mdahalo mjini Las Vegas.
Katika mdahalo huo wawili hao wamepambana vikali katika masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa silaha, utoaji mimba na uhamiaji haramu nchini humo.
Wawili hao waliovutana ni kuhusu uhusiano kati Marekani na nchini ya Urusi na silaha za nyuklia.
Donald Trump akitaka uhusiano kati ya Marekani na Urusi huku Hillary Clinton akikataa uhusiano na Urusi huku akisema Urusi ni hatari kwa Marekani.
Clinton kwa upande wake amesisitizia msimamo wake kuhusu sheria kali katika umiliki wa silaha nchini Marekani.
Kwa upande wake Donald Trump alimshutumu Bibi Clinton kwamba amejinufaisha kwa fedha zisizo halali.
Huo ni mdahalo wa mwisho wa wagombea hao wa Republic na Democtratic kabla hawajaingia kwenye uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka huu.