Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ameuomba uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuwasaidia kutengeneza viti na meza kwa ajili ya walimu baada ya kukamilisha madawati.

Amesema inapomalizika changamoto moja huibua nyingine ambapo wadau wanapaswa kushirikiana ili kuondoa changamoto hizo kwenye sekta hiyo ya elimu.

“Wananchi wanapaswa kushirikiana na serikali katika kukabili changamoto hizo zinazoibuka baada ya nyingine kutatuliwa, hivyo nguvu zetu tuzielekeze kwa kuwasaidia walimu ili nao waweze kufundisha wakiwa kwenye mazingira mazuri,” alisema.

Meneja wa TFS wilaya ya Kibaha, Peter Nyahende alisema wameamua kutoa madawati hayo yenye thamani ya Sh milioni 11.2 kwa lengo la kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli ili kuhakikisha watoto hawakai chini.

Nyahende amesema wamekuwa wakishirikiana na halmashauri ambapo hivi karibuni waliwauzia mbao 130 kwa ajili ya kutengeneza madawati wakati utaratibu huo unaanza ambapo kwa sasa wameamua kutengeneza kabisa madawati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *