Aliyekuwa makamu wa rais Congo, Jean-Pierre Bemba amepatikana na hatia katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ya kuwahonga mashahidi.
Mapema mwaka huu Bemba alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadmu na kuhukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani.
Siku ya jana alihukumiwa kwa kuwashaiwshi mashahidi kwa hongo na kubadilisha ushahidi katika kesi hiyo.
Washirika wake wanne wa karibu pia wamepatikana na hatia.
Majaji wameamua kuwa mashahidi 14 wakuu katika kesi ya awali ya Bemba, walifunziwa nini cha kusema.
Bemba alihukumiwa Machi kwa uhalifu uliotekelezwa katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya kati mnamo mwaka 2002-2003.
Alituhumiwa kwa kushindwa kuvisitisha vikosi vya waasi vilivyowaua na kuwabaka watu.
Bemba alifungwa Juni na anakata rufaa kupinga hukumu aliyopewa.