Mkali wa miondoko ya hip hop nchini, Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi amesema walioanzisha tuzo za EATV ni watu sahihi kuanzisha tuzo hizo kwa sababu ni watunwanaojua mziki.
Nikki wa Pili amesema EATV kuanzishwa kwa tuzo ni sawa na mwanafunzi kukutana na mwalimu sahihi wa somo husika, kwani ana imani itainua sanaa ya Tanzania.
Nikki wa Pili amesema “Media ni mdau moja kwa moja wa muziki, mziki unapigwa hapo, movie zinaruka hapo, kwa hiyo nje ya kwamba hawa ni wadau lakini pia ni watu wenye ufahamu mkubwa sana, kwa hiyo nafikiri media kutoa tuzo ni kama mwanafunzi amekutana na mwalimu hasa wa lile somo, ni kitu kizuri ni platform yenye nguvu sana”,.
Nikki wa pili aliendelea kusema kuwa EATV AWARDS zitaongeza wasifu mkubwa kwa wasanii na thamani yao, pamoja na kuwafanya kutambulika duniani kwa kazi zao nzuri.
EATV Awards ni tuzo zilizoanzishwa na kituo cha EATV ambazo zinashirikisha nchi za Afrika Mashariki zikijumuisha sanaa ya muziki na filamu ambapo sherehe zake zinayatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City mwaka huu.