Corneille Nyungura ni mwanamuziki mwenye asili ya Rwanda ambaye kwasasa anaishi nchini Canada na kupewa uraia wa nchi hiyo baada ya kukimbilia huko kutokana na mauji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994.
Mwaka 1994 alikuwa na umri wa miaka 17 akiishi nchini Rwanda kwenye familia moja tajiri na ndoto yake ilikuwa ni ya kuwa muimbaji maarufu.
Lakini maisha ya Corneille Nyungura yalichukua mkondo mwingine kwa ghafla wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka mwaka 1994 wakati takriban watu 800,000 wa kabila la watusi na wahutu wachache wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Wakati kundi la wauaji lilipowasili nyumbani kwao, Corneille alijificha nyuma ya sofa wakati familia yake yote ilichinjwa.
Sasa yeye ni raia wa Canada na mmoja wa wanamuziki bora zaidi wa RnB kutoka nchini Rwanda na amekuwa akiimba kwa miaka 20 iliyopita
Akijaribu kukubaliana kile kilichotokea nchini mwake mwaka 1994, Corneille anasema kuwa na uoga wa kurudi nyumbani kwao.