Jumuia ya wanawake wa Chama cha wananchi CUF (JUKECUF) wamewataka baadhi ya viongozi wa siasa nchini kuacha kuingilia mgogoro wa ndani wa chama hicho.
Angalizo hilo limetolewa na Katibu wa wanawake CUF Bi Salama Masoud wakati akitoa tamko la Jumuia hiyo kuhusiana na vurugu zinazoendelea katika chama hicho.
Sambamba na hilo wamemuomba Katibu mkuu wa CUF Maalim Saif Sharif Hamadi arejee majukumu yake katika chama kikatiba ili wamalize tofauti zao.
Wametoa angalizo kwa UKAWA kuacha kuingilia mgogogro huo na usitumike kama kivuli cha kuingilia mambo ya ndani ya CUF.
Amesema wao wanamtambua Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF ni Prof.Ibrahim Lipumba na kumtaka katibu mkuu atoe mrejesho wa mafanikio cha changamoto zilizotokana na ushirikiano wa UKAWA, kwakua wanayo haki wanachama kujua faida na hasara za ushirikiano kabla hawajatoa baraka zakuendelea na umoja huo.