Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, Hermy B kutokea studio za ‘B Hits’ amefunguka na kusema kuwa watayarishaji wengi wa muziki nchini ni masikini na maisha yao hayafanani kabisaa na majina yao.
Hermy B amesema hayo kupitia account yake ya twitter na kudai kuwa watayarishaji wengi wa muziki wa bongo hawana tofauti na watu wanaobeba mizigo (Makuli) kwani wanafanya kazi kubwa sana lakini kipato wanachopata kutokana na kazi hiyo ni kidogo mno kiasi cha wengi kuwa na maisha ya chini ukilinganisha na majina yao.
Haermy B ameandika maneno haya kwenye akaunti yake ya Twitter “Producer Wa muziki Tanzania hana tofauti na kuli anayebeba mizigo bandarini…anatumia nguvu nyingi lakini kipato hafifu…wengi ni maskini” aliandika Hermy B
Kwa upande mwingine Hermy B amesema kuwa hana uhakika kama baadhi ya wasanii wa bongo wanakumbuka kufanya Investement ili kuzidi kujiongezea kipato kutokana na pesa ambazo wamekuwa wakipata kupitia muziki wao na dili za hapa na pale.