Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani kwa mwaka 2016.
Rais huyo anaingia kwenye orodha ya viongozi wengine duniani waliowahi kushinda tuzo hiyo.
Mpaka sasa viongozi 25 wa juu wa serikali duniani kote wamewahi kushinda tuzo na 14 kati yao walikuwa madarakani.
Sababu kubwa ya Rais Juan kushinda tuzo hiyo ni juhudi za rais huyo kutaka kumaliza mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 220,000 huku wengine zaidi ya milioni sita wakikimbia makazi yao.
Tuzo hiyo ilianza kutolewa tangu mwaka 1901- hadi sasa.