Madaktari wa hospitali ya taifa ya Muhimbili waliomfanyia uchunguzi wa kina kijana Said Ally aliyejeruhiwa sehemu mbalimbai za mwili wake ikiwemo machoni, wametoa majibu kuhusu uchunguzi huo ambao ulilenga kutafuta uwezekano wa kumsaidia kuona tena na kudai kwamba, kijana huyo hatoweza kuona.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ofisini kwake na kuthibitisha hayo yaliyosemwa na madaktari waliomfanyia uchunguzi.

Makonda amesema kwamba “Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote,”.

Vile vile mkuu wa mkoa amesema “Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake,”.

Pia Makonda amesema serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni kumi kama sehemu ya mtaji wake.

 Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said Ally alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja,”.

Kupitia Instagram pia, Makonda ameandika: Watanzania wengi tulitamani Said uone tena ila tumeshindwa, tuna mwachia Mungu.      

Kwa upande mwingine mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo ‘Scorpion’ anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukamatwa na kupandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Ilala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *