Tanzania imetajwa na Benki ya Dunia kuwa miongoni mwa mataifa machache duniani ambayo yamefanikiwa kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini.

Kwenye ripoti ya benki hiyo kuhusu usawa duniani, Tanzania imeorodheshwa pamoja na Cambodia na Brazil kama nchi tatu zilizopiga hatua sana.

Nchini Tanzania, ripoti hiyo inasema, ufanisi ulipatikana katika kipindi ambacho taifa hilo lilipata ukuaji thabiti wa uchumi wa kiwango cha wastani cha asilimia 6.5 kila mwaka kati ya 2004-2014.

Kwenye kipimo cha pengo kati ya maskini na matajiri, Tanzania iliimarika kutoka alama 39 mwaka 2007 hadi chini ya alama 36 mwaka 2012.

Kipimo cha wastani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara mwaka 2015 kilikuwa alama 45.1.

Hatua zilizopigwa na Tanzania katika kupunguza pengo kati ya maskini na matajiri kipindi hiki kifupi ni cha kutia moyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *