Rais wa shirikisho la soka dunia (FIFA), Gianni Infantino ameshauri kuongezwa kwa timu zitakazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48 ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo.
Infantino ameshauri kuwa timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa huku zingine zikiendelea.
Timu 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.
Infantino amesema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.
Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.