Klabu ya soka ya Antalyaspor ya Uturuki imemjumuisha kikosini mshambuliaji wake Samuel Eto’o katika mchezo unafouata dhidi ya Galatasaray hii ikiwa ni kinyume na matarajio ya wengi.

Mwenyekiti wa Antalyaspor Ali Safak Ozturk amesema kuwa Eto’o ameomba radhi kutokana na kosa lake alilofanya kipindi cha nyuma.

Hivi karibuni mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon aliwekwa nje ya kikosi hicho kutokana na kutoa maneno ya kibaguzi kwa uongozi wa klabu hiyo aliyoyaweka katika mtandao wake wa Instagram akisema kuwa ”yamkini baadhi ya watu hawaniheshimu kwa sababu mimi ni mweusi”.

Eto’o ni mchezaji wa zamani wa Barcelona aliingia katika mgogoro na klabu yake hiyo ya Uturuki kutokana na kitendo cha kuandika taaifa kuhusu ubaguzi wa rangi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *